Pages

UKO FREE!!

Wednesday, 4 June 2014

Mdada mmoja mrembo sana alikuwa
kapewa talaka
na mumewe akahamia nyumba
aliyokuwa kapanga
MUTURI. MUTURI alipomuona
mpangaji mpya roho yote
ikamtoka. Akajitahidi kila njia
kumuonyesha kuwa
nae yupo na ni bachela, mdada
akawa anaendelea
na shughuli zake bila hata
kuonyesha dalili za kumwona
MUTURI. Jioni moja MUTURI akiwa
kapumzika
akasikia hodi kwenye chumba chake,
alipofungua
akakutana uso kwa uso na mdada
mpangaji,
kapendeza sana na akiwa kavaa
kimini cha nguvu;
MDADA: Samahani kaka MUTURI,
yaani nimekaa muda
mrefu mpweke nimeona leo lazima
nitoke nikajirushe kidogo kisha
nipate bwana niondoe
uchovu. Vipi we uko free?
MUTURI: Mimi sana tu niko free sina
kitu chochote
ninachofanya jioni hii, yaani niko
free kabisa si
unaona mwenyewe niko free sina
ishu kabisaaa
MDADA: Loh nakushukuru sana kaka
yangu, basi ngoja nikuletee watoto
wangu ushinde nao
mpaka ntakaporudi

0 comments:

Post a Comment

 
Shinekenya © 2014 Designed by Madebe ,