Pages

Jicho pevu on Mpeketoni saga

Thursday, 19 June 2014

Amid Kenya’s trying times,
investigative journalist Mohamed
Ali wrote the president a letter in
Swahili to ail his sentiments on
behalf of Kenyans. Much has been
said and done about the insecurity
issue in the country, take time to
go through the letter below:
Rais,
Habari ya siku nyingi?
Jina langu ni Mohammed Ali,
mwandishi wa habari ya
runinga ya KTN. Mara ya
mwisho kuonana naye ilikua
wakati wa kampeni za
uchaguzi mkuu uliopita huko
Mombasa katika shule ya
msingi ya Khadija. Ulikua
mchangamfu kando na ahadi
chungunzima kwa Wakenya.
Ahadi za tarakilishi za bure
kwa wanafunzi wa darasa la
kwanza, kutoa nafasi za kazi
milioni moja kila mwaka kwa
vijana, kuekeza katika
usalama wa kitaifa miongoni
mwa ahadi zingine. Lakini,
kwa hivi sasa bwana rais
nahofia ahadi hizo zimekua
tasa.
Barua yangu inaanza na
maswala ya usalama ambayo
nimeyapa kipau mbele.
Kwanza kabisa nauliza, “Uko
wapi? Hatukuoni bwana
Rais.”
Wakenya wanashabuliwa kila
mara na kuuliwa kinyama.
Walioponea wamebagi na
vilema vya maisha.
Shambulizi la Westgate na
ahadi ya serikali yako
zilionekana kama hekaya za
Abunuasi. Uliowapa
majukumu ya kutulinda wako
wapi? Kuanzia Mkurugenzi wa
NIS, Michael Gichangi,
Inspekta Jenerali wa Polisi,
David Kimaiyo, Mkurugenzi wa
CID, Ndegwa Muhoro,
Kamanda wa GSU, Kitili
Mboya, Waziri wa Usalama wa
Ndani, Joseph Ole Lenku na
Mkuu wa Majeshi, Julius
Waweru Karangi.
Ukweli wa mambo ni kwamba
Wakenya wanahisi kuwa nyote
mmelala.
Usalama umegeuzwa na kuwa
mchezo wa tufe. Tumejisahau
kiasi cha hata kuonyesha siri
zetu za ndani kwa maadui
zetu. Hatujui tunapigana na
nani.
Katika kazi yangu ya uandishi
wa habari, nimezungumza na
wadadisi wa maswala ya
usalama na bwana Rais wengi
wao wanahisi twapigana
wenyewe kwa wenyewe. Na
iwapo si wenyewe kwa
wenyewe basi twafukuzana na
kivuli cha fimbo ambacho
hakisitiri jua.
Badala ya kuua magaidi
tunajiua wenyewe kwa
wenyewe. Kwa kweli hatuwezi
shinda vita hivi ikiwa
twaumizana wenyewe kwa
wenyewe badala ya
kuungana. Mara tunaambiwa
ni MRC, mara ni Mungiki,
mara magaidi, maragodoro na
sasa waziri wako Ole Lenku
ana mapya zaidi.
Waswahili wanasema “Bata
ata umlishe mawe bado
atahara”. Bwana Rais,
tumwamini nani?
Bwana Rais, majuzi uliingia
na taswira mpya kabisa katika
uwanja wa Nyayo; magari ya
kujikinga na risasi na
usalama zaidi. Hii, si kawaida
tangu uongozi wa Hayati
Mzee Jomo Kenyatta, Daniel
Toroitich arap Moi na Mwai
Kibaki. Iwapo wewe unahofia,
je sisi walalahoi tutahisi vipi?
Mauaji ya Mpeketoni ni sawia
nay ale ya Tana River. Damu
ya wana Mpeketoni inalilia
haki. Kina mama wamechwa
bila watoto na waume huku
watoto wakisalia mayatima
kwa kosa la serikali
walilolichagua ki katiba,
serikali iliyowaahidi
kuwalinda pamoja na mali
zao. Mauaji ya kiholela
yanazidi kugonga vichwa vya
habari, baadhi ya walinda
usalama wameamua wao ndio
majaji na mawakili kwa
Wakenya wanyonge wasio na
mtetezi.
Bwana Rais, wakenya wanalia;
kuanzia Easatleigh, Baragoi
hadi Mandera.
Nina machungu na mengi ya
kukueleza lakini muda
hauniruhusu. Kumbuka Kenya
ni jina, nchi ni sisi.
Ni hayo tu kwa sasa.
Shukran.

0 comments:

Post a Comment

 
Shinekenya © 2014 Designed by Madebe ,